Shirika la jeshi kupanua wigo wake

Nuzulack Dausen
May 23, 2017

Dodoma. Shirika la Mzinga limeanda mkakati unaokusudia kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao ya kijeshi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema hayo leo wakati akiwasilisha hotuba yake ya bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 bungeni.

Amesema mkakati huo pia unalenga katika kuongeza wigo wa shughuli za shirika kwa kuanzisha viwanda vipya vya kutengeneza baruti na kupanua mradi wa kutengeza mashine ndogo ndogo kwa ajili ya kuwaezesha wajasiriamali(wadogo wadogo na wa kati) kufanya uchakataji na kuongezea thamani ya mazao ya kilimo na misitu.

Wizara hiyo inaomba Bunge kuwaidhinishia Sh 1.72 trilioni Kati ya hizo Sh 1.5 trilioni ni matumizi ya kawaida na Sh 219 bilioni kwa ajili ya matumizi ya miradi ya maendeleo.

Nuzulack Dausen

Nuzulack Dausen ni Mkuu wa dawati la habari za takwimu wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Mwaka 2015 alishinda tuzo ya Mwandishi bora wa habari za Uchunguzi kwa upande wa magazeti zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Amejikita zaidi katika habari za biashara, uchumi, teknolojia na data.

MWANANCHIDataLab by Code for Tanzania